Habari za Punde

Elimu juu ya UVIKO 19 yafika Kizimkazi

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs )  Neema Lugangira akitoa Semina ya Uviko 19 kwa viongozi wa UWT Huko Kizimkazi Visiwani Zanzibar
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs ) akizungumza wakati akitoa Semina ya Uviko 19 kwa viongozi wa UWT Huko Kizimkazi Visiwani Zanzibar
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs ) Mh Neema Lugangira akizungumza wakati akitoa Semina ya Uviko 19 kwa viongozi wa UWT Huko Kizimkazi Visiwani Zanzibar
Washriiki wa Semina hiyo wakimsikiliza kwa Umakini Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs ) Mh Neema Lugangira  ambaye hayupo pichani wakati akitoa Semina ya Uviko 19 kwa viongozi wa UWT Huko Kizimkazi Visiwani Zanzibar

 NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR.


 MBUNGE wa Viti Maalumu CCM anaewakilisha Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira ametoa Elimu ya UVIKO 19 kwa Wenyeviti na Makatibu wa Matawi yote ya UWT, Kizimkazi, Makunduchi, Mkoani Kusini Unguja huku lengo likiwa kuwaongezea hamasa na uelewa sahihi kwenye ngazi ya jamii kuhusiana na Ugonjwa wa UVIKO19 na Umuhimu wa Chanjo ya UVIKO19.

Akizungumza wakati akitoa Elimu hiyo ikiwa ni katika Kuadhimisha Wiki ya UWT ambapo  Mbunge Neema alipata mwaliko maalumu, Alisema wameamua kutoa elimu hiyo ili kuweza kuwapa uelewa namna ya kujikinga na uviko 19 kwa kuhakikisha wanatumia hiari yao vizuri ya kupata chanjo ya uviko 19 ambazo zinatolewa maeneo mbalimbali kwani itawasaidia kukumbwa na ugonjwa huo ambao ni hatari. 

Alisema wameamua kufanya semina hiyo kwa viongozi wa kisiasa kutokana na kwamba wamekuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii na wanaishi miongoni  mwa jamii na hivi sasa ugonjwa wa uviko19 umevamiwa na upotoshaji mwingi hivyo jamii inahitaji elimu sahihi itakayowawezesha kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya kujikinga na kuwakingine wengine na ugonjwa huu hatari wa UVIKO19.

“Hivyo wanapopata elimu kwa viongozi wanaowafahamu wana imani nao watakapowaelewesha wataelewa ugonjwa upo na ni hatari na namna ya kuweza kujikinga naamini kupitia viongozi hao wataweza kuongeza hamasana” Alisema Mbunge Neema Lugangira.

Hata hivyo alisema ni muhimu  na uelewa jamii wa uviko 19 na usalama wa chanjo na kuwawezesha kuweza kutumia hiari yao vizuri kuweza kuchangua chanjo ya uviko 19 ambayo ni salama na hivyo kuepukana na kupata ugonjwa huo.

Semina hii Semina ilifanyika Jumapili tarehe 3/10/21 Kijiji cha Kizimkazi, Makunduchi alipozaliwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan. 

Aidha, Mbunge Neema Lugangira amesema akiwa kama Mbunge na Balozi wa Kitaifa wa UVIKO19 anatarajia kufikisha Elimu ya UVIKO19 kwa Viongozi wa Kiasiasa Mikoa mbalimbali nchini akianzia na Mikoa ambayo ipo hatarini zaidi hivyo anakaribisha Wadau wote kushirikiana nae katika kufanikisha Kampeni yake ya Elimu ya UVIKO19 kwa Jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.