Habari za Punde

MAJALIWA AZINDUA MRADI WA MAPANGO WA KANISA KATOLIKI WA MAPAMBANO DHIDI YA UVICO-19

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021.  Wengine kutoka kushoto ni Jane Manyahi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Cardinal Rugambwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na uzazi, Balozi wa Marekani nchini Donald Wright, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Godwin Mollel na kulia ni Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Cardinal Rugambwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na uzazi Dkt. Jane Manyahi (kulia) ambaye alitoa maelezo kuhusu vifaa mbalimbali ambavyo vimetolewa na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID) kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19 wakati wa uzinduzi wa mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021. wa pili kushoto ni Balozi wa Marekani nchini Donald Wright, wanne kushoto ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga na watano kushoto ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Stephano Msomba.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021. Kulia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga na katikati ni Balozi wa Marekani nchini Donald Wright

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Balozi wa Marekani nchini Donald Wright wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021. kushoto ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga na watatu kushoto ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Stephano Msomba.

 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.