Habari za Punde

Mapokezi ya Ndege Mbili za Airbus A220-300 za Air Tanzania Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Moja ya Ndege Mpya za Air Tanzania ya Airbu A220-300 ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.ikotokea Nchini  Canada. 
Ndege mbili Mpya za Air Tanzania Airbus A220-300 zikiongozana baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, wakati wa hafla ya mapokezi yake na kupokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi.  
Ndege Mbili Mpya za AIR Tanzania aina ya Airbus A 220-300 zikipokelea kwa heshima zote na kumwagia maji ikiwa ni ishara  ya mapokezi yake katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.  
Ndege Mbili Mpya za AIR Tanzania aina ya Airbus A 220-300 zikipokelea kwa heshima zote na kumwagia maji ikiwa ni ishara  ya mapokezi yake katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.  

Wananchi wa Zanzibar wakizipokea Ndege mbili za AIR Tanzania kwa kupiga picha za kumbukumbu  kupitia simu zao wakati zikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar zikitokea Nchini Canada.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kufungua Ndege Mbili Mpya za Air Tanzania aina ya A 220-300 Airbus, baada ya kuzipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.