Habari za Punde

Mbunge wa jimbo la Mkoani akabidhi misaada jimboni

MBUNGE wa Jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba Profesa Makame Mbarawa Mnyaa, akiwaeleza jambo walimu wakuu wa skuli ya Mkanyageni, Michenzani na Ngombeni B, pamoja na uongozi wa kituo cha afya Tasini, kabla ya kuwakabidhi bati, mbao na shilingi Laki tano, kwa ajili ya kuezekea mabanda hayo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MBUNGE wa Jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba Profesa Makame Mbarawa Mnyaa, akimkabidhi bahasha yenye shilingi Laki Tano kwa ajili ya uwezekaji wa banda la skuli, Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Ngombeni B Iddi Ameir Khamis, hafla iliyofanyika Katika skuli ya Msingi Michenzani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MBUNGE wa Jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba Profesa Makame Mbarawa Mnyaa (wa kwanza kulia), akiwakabidhi bati walimu wakuu wa skuli ya Michenzani, Mkanyageni na Ngombeni B, pamoja na uongozi wa kituo cha afya Tasini kwa ajili ya kuezekea, hafla iliyofanyika katika skuli ya Chokocho Wilaya ya Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MBUNGE wa Jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba Profesa Makame Mbarawa Mnyaa (wa pili kutoka kushoto), akiwakabidhi mbao za kuezekea walimu wakuu wa skuli ya Michenzani, Mkanyageni na Ngombeni B, pamoja na uongozi wa kituo cha afya Tasini kwa ajili ya kuezekea, hafla iliyofanyika katika skuli ya Chokocho Wilaya ya Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WATENDAJI wa kamati ya jimbo la Mkoani, wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya kuezekea mabanda ya skuli mbali mbali zilizomo ndani ya jimbo hilo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.