Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na kufanya mazungumzo na Rais Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiya Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, alipowasili Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo akiwa Zanzibar kwa ziara ya Siku moja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiya, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu wakati ukipingwa wimbo wa Taifa wa Burundi, Zanzibar, Tanzania na wa Afrika Mashariki,kabla ya kuaza kwa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 23-10-2021, akiwa Zanzibar kwa ziara ya siku moja.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mama Angeline Ndayishimiye (kulia kwake) wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar wakati wa ziara ya siku moja ya Rais wa Jamhuri ya Burundi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe Evariste Ndayishimiye.(kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, wakati wa ziara yake ya Siku moja Zanzibar.(Picha na Ikulu)  
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa zawadi Maalum na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mama Angeline Ndayishimiye, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, akiwa Zanzibar kwa ziara ya siku moja na Mumewe Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye.(hayupo pichani) (Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Kasha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mama Angeline Ndayishimiye, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, akiwa Zanzibar kwa ziara ya siku moja na Mumewe Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye.(hayupo pichani) (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar,mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe Evariste Ndayishimiye, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, akiwa Zanzibar kwa ziara ya Siku moja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe Evariste Ndayishimiye, baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula maalum cha mchana alichomuandalia mgeni wake katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, akiwa Zanzibar kwa ziara ya Siku moja.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.