Habari za Punde

Utoaji wa Tuzo za Rais Kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda Nchini Tanzania.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda nchini (CTI) Paul Makanza mara baada ya kumalizika hafla ya utoaji tuzo za Rais za wazalishaji bora wa viwandani. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa juu wa jumla wa tuzo za Rais za wazalishaji bora wa viwandani  wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo uliofanyika Serena Jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhi tuzo kwa mshindi wa kwanza wa jumla wa tuzo za Rais za wazalishaji bora wa viwandani ambaye ni Tanga Cement wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo uliofanyika Serena Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wazalishaji wa bidhaa za viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais za wazalishaji wa viwandani iliofanyika Serena Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wazalishaji wa bidhaa za viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais za wazalishaji wa viwandani iliofanyika Serena Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema bado kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini ni mdogo na hivyo kuitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Shirikisho la Viwanda (CTI) kufanya tafakuri ya kina kupata suluhu ya changamoto zinazokwamisha Sekta hiyo.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani nchini, hafla iliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Amesema bado bidhaa zinazozalishwa hapa nchini hazijakidhi mahitaji ya wananchi na baadhi kutokidhi viwango vya soko hivyo kuendelea kuagiza bidhaa za viwandani kutoka nje ya nchi. Makamu wa Rais ametaja baadhi ya bidhaa zilizotumia gharama kubwa kwa kuagizwa kutoka nje ya nchi mwaka 2020 kama vile shilingi bilioni 200 kutumika kuagiza bidhaa za vitambaa ikiwa pamba inazalishwa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.