Na Maulid Yussuf WEMA. MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Viongozi mbalimbali nchini, wametakiwa kushirikiana hasa katika ngazi za shehia kwa kuwafichua watoto wliitoroka Skuli ili kuwarudisha kupata haki yao ya Elimu kikatiba.
Akizungumza kikao cha uhamasishaji wa mradi wa kuwarudisha watoto Skuli kwa Viongozi wa ngazi mbali mbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ukumbi wa Skuli ya Dkt Ali Mohammed Shein, Kaimu Katibu Tawala Wilaya Mghribi A' bwan Mustafa Hassan Mkadam amesema kumeonekana kuwepo vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimekuwa vikiathiri sana watoto .
Aidha amewataka washiriki kuyapokea vyema maelekezo watakayopatiwa na kuyatekeleza kwa vitendo na kuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko kwa kuwaokoa watoto ambao ndio tegemeo kubwa la Taifa hapo badae.
Amesema kwa mujibu wa Taarifa alizozipata katika Mkoa wa Mjini Magharibi, kuna vijana 8801 ambao wametoroka Skuli, hivyo imani yake baada ya kupata taarifa na maelekezo ya mradi huo wataweza kushirikiana kusaidia kuwarejesha watoto hao ili wapte elimu kwa mendeleo ya Taifa.
Nae Mkurugenzi Idara ya Elimu Mbadala na watu wazima bi Mashavu Ahmada Fakih amesema kuanzishwa kwa mradi wa kuwarejesha watoto Skuli kutasaidia kupunguza watoto wa mitaani katika visiwa vya Zanzibar.
Amesema lengo la kikao hicho ni kuona kila mmoja anawajibu wa kuwasaidia watoto hao ili wapate elimu ambayo itawasaidia kuondosha tatizo la watu wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika.
Bi Mashavu amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imedhamiria katika ilani ya chama cha Mpibduzi kuhkikisha watoto wote wanapata elimu ambayo itawasadia katika maisha yao ya baadae.
Hivyo amesema ni wajibu wa washiriki hao kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa hli ya juu ili malengo ya Serikali pamoja na mradi huo katika kuwapatia watoto elimu uweze kufikiwa.
Nae Mratibu wa Mradi huo bw Mzee Shirazi Hassan amesema mradi huo ameshaanza kutekelezwa kwani mpaka Sasa wamefanikiwa kuwarejesha watoto elfu 2600 Kati ya wtoto elfu 35732 ambao hawakupata elimu, hivyo ameiomba jamii kushirikiana kwa lengo la kuwapatia elimu ambayo ni haki yao kikatiba.
Nao washiriki wa kikao hicho wamesema wapo tayari kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kufikia lengo la kuona kila mtoto ananufaika na elimu
Mradi wa kuwarejesha watoto Skuli unalenga kuwarudisha watoto Skuli waliokuwa na umri wa miaka 7 hadi miaka 14 katika visiwa vya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment