Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Amezindua Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum  ya Wavulana Nachingwea, Oktoba 25, 2021. Kulia ni Mbunge wa Nachingwea , Dkt. Amandus Chingwile na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji Sahani ambaye  alitoa maelezo kuhusu michoro ya Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana  Nachingwea  kabla ya  Waziri Mkuu kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji  Sahani   (kulia) kuhusu  ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Oktoba 25, 2021.  Wa tatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Lindi,  Zainab Telack.
Muonekano wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavula Nachingwea ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake, Oktoba 25, 2021. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.