Habari za Punde

DPP mpya afika Pemba kujitambulisha

MWENDESHA Mashataka wa Serikali Pemba Asiya Ibrahim Mohammed, akimvisha koja Mkurugenzi wa Mashataka Zanzibar Salma Ali Hassan, mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Pemba, kwa ajili ya kujitambulisha kwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza toka kuteuliwa
JAJI wa Mahakama Kuu Zanzibar Muumini Khamis Kombo, akizungumza katika mkutano wa kumtambulisha mkurugenzi mpya wa Mashtaka Zanzibar na kumkabidhi ofisi na wafanyakazi upande wa Pemba, hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Madungu Chake Chake.
JAJI wa Mahakama Kuu Zanzibar Muumini Khamis Kombo, akimkabidhi Muongozo wa Uwendeshaji wa Mashataka Zanzibar wa 2015 kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Salma Ali Hassan, ikiwa ni makabidhiano ya ofisi yake mpya uapnde wa Pemba, hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Madungu Chake Chake
MKURUGENZI wa Mashataka Zanzibar Salma Ali Hassan, akizungumza na watendaji wa Ofisi yake Pemba wakati wa mkutano wa kujitambulisha kwake na kukabidhiwa vitendea kazi, hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Madungu Chake Chake
MWENDESHA Mashtaka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pemba Asiya Ibrahim akitoa neno la shukurani kwa mkurugenzi mpya wa Mashtaka Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kujitambulisha kwake kwa wafanyakazi wa ofisi ya Pemba.

WAFANYAKAZI wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Pemba, wakiwa katika mkutano na mkurugenzi wao mpya wa Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar, aliopofika kujitambulisha kwa watendaji wa ofisi yake Pemba.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.