Makamu wa Pili wa Zanzibar Mhe. Hemed akimfariji Rais msataafu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake Shein Mohamed Shein Kilichotokea Jana nyumbani kwake Chukwani.
Makamu wa Pili wa Zanzibar Mhe. Hemed akimfariji Rais msataafu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake Shein Mohamed Shein Kilichotokea Jana nyumbani kwake Chukwani.
Mhe. Hemed akiwa pamoja na waumini wa Dini ya kislamu wakishiriki katika ibada ya sala ya maiti iliofanyika katika masjid QUBA uliopo kwa Boko kufuatia kifo cha kaka wa Rais mstaafu wa awamu ya saba Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na waumini wa Dini ya kislamu wakishiriki katika ibada ya sala ya maiti iliofanyika katika masjid QUBA uliopo kwa Boko kufuatia kifo cha kaka wa Rais mstaafu wa awamu ya saba Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewaongoza wanafamilia na waumini kuustiri mwili wa marehemu Shein Mohamed Shein Kaka wa Rais mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya Saba katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewaongoza wanafamilia na waumini kuustiri mwili wa marehemu Shein Mohamed Shein Kaka wa Rais mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya Saba katika makaburi ya mwanakwerekwe.
Na Kassim Abdi, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameongoza maziko ya Shein Mohamed Shein Kaka wa Rais Mstaafu wa awamu ya saba Zanzibar.
Mhe. Hemed amejumuika na wanafamilia pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kuustiri mwili wa marehemu Shein Mohamed Shein katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Mahgharibi “B” Unguja.
Harakati izo za kuustiri mwili wa marehemu Shein Mohamed Shein zimehudhuriwa na wanafamili, Mufti Mkuu wa Zanzibar Samahatu Sheikh Saleh Omar Kaabi, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la wawakilisha Zubeir Ali Maulid, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Wakati wa Adhuhuri, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alishiriki ibada ya Sala ya kumsalia maiti katika Masjid QUBA uliopo kwa Boko.
Mapema Asubuhi Mhe. Hemed alifika nyumbani kwao marehemu Shein Mohamed Shein kwa ajili ya kuipa pole familia pamoja na kumuombea dua marehemu huyo.
No comments:
Post a Comment