Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu Dk Shein kufuatia kifo cha kaka yake

 

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Durban, Afrika Kusini                                            15.11.2021

---

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba Mheshimiwa  Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake  Mzee Shein Mohamed Shein kilichotokea jana (Novemba 14,2021).

 

Katika salamu hizo za pole,  Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa kwake na kifo hicho  na kumtakia  pole na ustahamilivu Rais Mstaafu Dk. Shein yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

 

Rais Dk. Mwinyi na familia yake wamemuomba  Mwenyezi Mungu amjaalie Marehemu Mzee Shein Mohamed Shein amlaze mahala pema peponi, Amin.

 

Rais Dk. Mwinyi  ametoa salamu hizo akiwa Jijini Durban, nchini Afrika Kusini akisihiri ufunguzi wa Mkutano wa Maonyesho ya Kukuza Biashara baina ya nchi za  Afrika.

 

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.