Habari za Punde

Amref Health Africa yatoa vifaa vya kusaidia utekelezaji wa utoaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko

MWAKILISHI kutoka Amref Health Africa Tanzania Dk.Atuganite Musyani, akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi GHSA, kwa Masheha na watu wa afya, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya kusaidia utekelezaji wa utoaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

NAIBU Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk.Salim Slimu, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kusaidia utekelezaji wa utoaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MWAKILISHI kutoka Amref Health Africa Tanzania Dk.Atuganite Musyani (kushoto) na Mwakilishi kutoka CDC Jane Kitalile wakifuatlia kwa makini hafla ya kukabidhi kukabidhi vifaa vya kusaidia utekelezaji wa utoaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

AFISA Mdhamini Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Pemba Dk.Yakub Mohamed Shoka, akitoa nasaha zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kusaidia utekelezaji wa utoaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MKUU wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakar, akizunguza na Msheha na Watendaji wa Afya Pemba katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kusaidia utekelezaji wa utoaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MWAKILISHI kutoka Shirika la Amref Health Africa Tanzania Dk.Atuganite Musyani na Mwakilishi kutoka CDC Jane Kitalile, wakimkabidhi kompyuta Mkuu wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakari, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa magonjwa ya mripuko na matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, 

MKUU wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakari (kulia) akimkabidhi DMO wa Wilaya ya Micheweni Mkubwa Habibu Khamis, Mashine ya kuchapisha ( Printer) kwa ajili ya kukusanyia taarifa mbali mbali za Magonjwa ya Mripuko na Matukio yenye athari kiafya katika jamii, hafla iliyofanyika Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.