(PICHA NA MARYAM KIDIKO – MAELEZO .)
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 14/01/2022.
Kampuni inayochunguza vinasaba kutoka Marekani imesema ina azma ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala ya utafiti wa vinasaba
.
Akiyasema hayo Mwenyekiti wa Kampuni ya kuchunguza vinasaba ( 54gene,Ine.) Dr Abasi Eneobong, alipofika na ujumbe wake, kuonana na Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe.Nassor Ahmed Mazrui, huko ofisini kwake, Mnazimmoja.
Alisema azma ya ujio huo ni kushirikiana na Wizara ya Afya katika masuala ya utafiti wa vinasaba ili kufanyakazi kwa pamoja katika uchunguzi huo.
Aidha alisema lengo la mazungumzo yao ni kufunga Mkataba wa mashirikiano ya pamoja katika utafiti wa vinasaba (Private, Public, Partneship,PPP) ambao unatarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo.
Nae Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema uchunguzi wa vinasaba itasaidia kupata dawa sahihi za kutibu maradhi mbali mbali katika jamii.
“Kwa vile Zanzibar ni kisiwa,tumechanganya damu za watu tofauti kutoka nchi mbali mbali za Arabuni, India, Uzunguni, China na Afrika uchunguzi wa vinasaba utasaidia kutibu” alisema Waziri.
.
Alifahamisha kuwa hii ni fursa azimu ya Wizara ya afya ambayo iliingojea kwa muda mrefu ya kuimarisha maabara kubwa ya utafiti iliopo Binguni .
Alieleza Zanzibar itakuwa Makao Makuu ya uchunguzi kutokana na ushirikiano wa kampuni hiyo na kuifanya iwe na hadhi ya kimataifa jambo ambalo litasaidia Wazanzibar kupata mafunzo ya utafiti pamoja na fursa za ajira ..
Kampuni ( 54gene,Ine.) ina matawi yake kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Nigeria,Kenya, Marekeni Londan na nchi nyengine.
No comments:
Post a Comment