Habari za Punde

Mhe Hemed aagiza kufanyiwa matengenzo ya haraka bombma liliposuka

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akiwa pamoja na Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mheshimiwa Suleiman M. Makame, na viongozi wengine wakishuhudia bomba la maji safi na salama lililopasuka eneo la Lumumba

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dr Salha Mohamed Kassim akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais kuhusu bomba la maji safi na salama lililopasuka eneo la Lumumba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akitoa maelekezo ya kufanyiwa ukarabati wa haraka bomba la maji safi na salama lililopasuka, alipotembelea kukagua bpmba hilo eneo la Lumumba

Picha na – OMPR 

Na Abdulrahman Khamis OMPR

Ipo haja kwa wakandarasi wanaoendelea na ujenzi wa Miradi ya maendeleo, kushirikiana na mamlaka mbali mbali ili kuepusha uharibifu wa miundombinu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo alipotembelea na kukagua Bomba la maiji safi na salama  lililopasuka lililopo eneo la Lumumba Jijini Zanzibar.

Amesema serikali imejipanga kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi,  ambapo wakandarasi wanaopewa Miradi hiyo ni vyema kujua maeneo yaliyopita Miundombinu hasa ya maji ili kuzuwia kutokea kwa athari ya aina yoyote ile.

Amesema kupasuka kwa Bomba hilo kumepelekea wananchi wa maeneo mbali mbali ya wila ya mjini kukosa huduma hiyo, ambapo amemtaka mkandarasi huyo kulipa gharama zote za Kurudisha huduma hiyo ikiwemo ya vifaa na gharama nyenginezo.

Mhe. Hemed ameeleza kuwa serikali inatoa gharama kubwa kwa kuboresha Miundombinu ya maji ili wananchi wapate huduma hiyo kwa wakati bila ya kikwazo, na kuwataka wananchi kwa ujumla kuilinda Miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka mafundi wanaosimamia ujenzi wa bomba hilo kuwajibika ipasavyo ili huduma hiyo irejee kwa wakati sambamba na kumtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha mafundi hao wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Aidha Mheshimiwa Hemed amewashukuru wananchi wa maeneo ya Mjini kwa ustahamilivu wao tokea kupasuka kwa Bomba hilo na kuwataka kuendelea kuwa na subira wakati mafundi wanaendelea na zoezi hilo.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameushukuru uongozi wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kwa hatua za awali walizochukua mara baada ya kupata kadhia hiyo,  na kuwataka kuendelea kutoa  mashirikiano ili kuhakikisha wananchi hawasumbuki katika kupata huduma hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) Dr Salha mohammed  Kassim amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa, hatua ya awali walioichukua mara baada ya kupata Taarifa ya kupasuka kwa Bomba hilo ni kuyafunga maji ili kupunguza kasi ya kupotea kwa maji hayo.

Aidha Dr Salha mesema bomba hilo linasambaza maji kutoka saateni kupeleka katika shehia mbali mbali za mjini ilikuwemo michezani, kikwajuni na maeneo mengine ya jirani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mheshimiwa  Rashid simai Msaraka amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuendelea kuwajali wananchi wake na kuwataka wananchi wa wilaya Mjini kuendelea kuwa wastahamilivu kwa kipindi kifupi na kuhakikisha huduma hio inapaikana kwa muda mfupi ujao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.