Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi amefungua madarasa sita ya skuli ya msingi Sebleni

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa kitamba kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Madarasa Sita ya Skuli ya Msingi ya Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,na (kulia kwa Mbunge) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa kitamba kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Madarasa Sita ya Skuli ya Msingi ya Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil,Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kingozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuyafungua Madarasa Sita mapya ya Msingi ya Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe.Simai Mohammed Said, Mwali Mkuu wa Skuli ua Msingi Sebleni na Mwakilishi ya Jimbi la Kwahani Mhe Abdalla Rashid Abdalla na (kulia kwa Rais) Mbunge wa Jimbo la Kwahani Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mistafa Kitwana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kwahani Mhe.Ahmada Yahya Abdulwakil akitowa maelezo ya moja ya madarasa Sita mapya ya Skuli hiyo yaliojengwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani, baada ya kuyafungua leo 7-1-2022, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwapungua mkono Wananchi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi ya Sebleni.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.