Habari za Punde

Hafla ya ufunguzi wa madarasa matatu ya kusomea kwa wananchi wa skuli ya Kiwani Msingi

MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, akifungua kanga kuashiria ufunguzi wa madarasa matatu ya kusomea kwa wananchi wa skuli ya Kiwania Msingi, madarasa hayo yamejengwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, huku viongozi mbali mbali wakishuhudia wakiwemo Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Kiwani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MWAKILISHI wa Jimbo la Kiwani Mussa Fumu Mussa, akizungumza na wananchi wa Kiwani katika hafla ya kukabidhi madarasa matatu ya kisasa ya kusomea wananchi wa skuli ya Kiwani, yaliojengwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza na wananchi wa Kiwani kupitia Simu ya Mbunge wa Jimbo hilo wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa matatu ya kusomea wanafunzi, yaliojengwa na Makamu wa huyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo, wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, huku viongozi mbali mbali wakishuhudia wakiwemo Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Kiwani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, akizungumza na wananchi wa Kiwania wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa matatau ya kusomea wanafunzi, yaliyojengwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja(kushoto), akimkabidhi kaimu afisa mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mwalim Harifa Bakar Waziri, madarasa hayo yaliojengwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MUONEKANO wa baadhi ya madarasa yaliyojengwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MUONEKANO wa baadhi ya viti na meza za kukalia wanafunzi wa skuli ya msingi Kiwani, vilivyomo katika madarasa matatu ya kusomea yaliojengwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoiweka kwa skuli hiyo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.