WAZIRI wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita ameupongeza Mkoa wa Kusini Unguja kwa jitihada na uzalendo wa kuratibu Mwenge wa uhuru na kuleta hamasa kubwa katika Mkoa huo.
Akizungumza na uongozi wa Mkoa huo mara baada ya kukabidhi kombe na cheti ikiwa ni ishara ya kuzindua mwenge wa uhuru katika uwanja wa Mwehe Makunduchi, hafla iliyofanyika huko ukumbi wa wizara ya habari migombani .
Alisema Mkoa huo umeleta hamasa kubwa kutokana na juhudi zilizofanywa kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo katika kuimarisha shughuli za Kitaifa .
Aidha amemuomba Mkuu wa Mkoa kuendelea kushirikiana katika masuala mbali mbali hasa ya vijana katika kuwaletea maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema Mwenge wa Uhuru umewapa historia katika mkoa huo, sambamba na kuendelea kushirikiana katika shughuli za kitaifa ili kuona zinakwenda kwa ufanisi.
Katibu wa Mkoa wa Kusini Unguja Salum Kassim Ali amesema haikuwa rahisi lakini maandalizi mazuri,uweledi,ushirikiano na waratibu kutoka tanzania bara na wananachi yameweza kufanikisha ipasavyo.
No comments:
Post a Comment