Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na uongozi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Bw. Sabasaba .K. Moshingi (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 3-3-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Bw. Sabasaba Moshingi.(kulia kwa Rais) akitowa maelezo ya huduma zinazotolewa na Benki hiyo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw.Sabasaba Moshingi (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana Ujumbe wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
(Picha na Ikulu) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.