Habari za Punde

KINANA ASEMA ZIARA YA RAIS SAMIA MAREKANI NI MUHIMU KWA UCHUMI.

Makamu Mwenyekiti CCM bara Comrade Abdulrahman Kinana akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama hicho mkoani Kilimanjaro katika ukumbi ofisi za chama mjini Moshi katika Ziara yake ya kujitambulisha Pamoja na  kukagua Uhai wa Chama Mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amempongezq Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kufanya kazi kubwa kuwaletea wananchi maendeleo katika kupindi cha mwaka mmoja tu alichokaa madarakani.

Amesema kwa sasa Rais yuko katika nchini Marekani  ambapo amesema ziara hiyo imemkutanisha na viongozi wakubwa akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ambaye nchi yake Ina ushawishi mkubwa duniani.

Kinana ameyasema mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa wana CCM wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.

"Sasa hivi anafanya ziara nje huko, kwa wafadhili, watoa mikopo, ili tuweze kupata fedha nyingi zaidi kwa maendeleo ya taifa letu.

"Rais yuko Marekani, ameonana na Makamu wa Rais wa Marekani. Marekani ni nchi kubwa, Marekani Ina kauli duniani, Marekani ni mshiriki wetu wa maendeleo katika sekta mbalimbali zinazowagusa wananchi," amesema.

Amesema Rais Samia pia amekutana na viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha duniani (IMF), Taasisi ambazo ni washirika muhimu wa maendeleo na uchumi wa Tanzania, hivyo anastahili pongezi.
Makamu Mwenyekiti CCM bara Comrade Abdulrahman Kinana akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama hicho mkoani Kilimanjaro katika ukumbi ofisi za chama mjini Moshi katika Ziara yake ya kujitambulisha Pamoja na  kukagua Uhai wa Chama Mkoani humo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  (CCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka akisisitiza jambo katika Mkutano wa Makamu Mwenyekiti CCM bara Comrade Abdulrahman Kinana mkoani Kilimanjaro katika ukumbi ofisi za chama mjini Moshi katika Ziara yake ya kujitambulisha Pamoja na  kukagua Uhai wa Chama Mkoani humo.
Makamu Mwenyekiti CCM Kinana akimsalimia Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Moshi Bi Jenifer Sudi  kwenye mkutano wa ndani wa  katika Ziara yake ya kujitambulisha Pamoja na  kukagua Uhai wa Chama Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.