Habari za Punde

Ipo haja kwa Wazanzibari kuungana ili kurudisha Hadhi na Heshima ya Zanzibar.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini wa masjid jumuiya chukwani buyu alipojumuika na waumini wa mskiti huo katika ibada ya sala ya ijumaa na kuwataka kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za kuijenga zanzibar yenye maendeleo. 

Waumini wa Masjid Jumuiya Chukwani Buyu wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla alipojumuika nao katika ibada ya sala ya ijumaa.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa Wito huo alipojumuika na Waumini wa Masjid Jumuiya uliopo Chukwani Buyu Wilaya ya Magharibi "B" katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Alhajj Hemed ameeleza kuwa Azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuijenga Zanzibar yenye Maendeleo na kuwataka Wananchi kuwa Mstari wa mbele katika kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua ya kimaendeleo.

"Sote tua wajibu wa kusimamia ujenzi wa Zanzibar tushikamane kumsaidia Rais Dkt Mwinyi ili tupate matokeo chanya katika Nchi yetu"

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Zanzibar yenye Amani itapelekea kupata maendeleo katika kila nyanja pamoja na kuwavutia wawekezaji kuja kuweza kwa lengo la kuisaidia Serikali katika kufikia malengo iliyojiwekea.

Alhajj Hemed ameendelea kuwaeleza Wananchi kuwa Serikali inajitahidi kumaliza changamoto mbali mbali zinazowakabili Wananchi wake ikiwemo migogoro ya Ardhi pamoja na kusogeza huduma za kijamii karibu na Wananchi.

Akizungumzia suala la Miradi ya maendeleo Mhe. Hemed ameeleza kuwa fedha zilizotengwa kwa ujenzi wa miradi hiyo Serikali inazisimamia na haitamvumilia yoyote atakaejaribu kufanya ubadhirifu wa fedha hizo ambapo tayari wapo walioanza kuchukuliwa hatua za Kisheria ili kudhibiti ubadhirifu huo.

Nae Maalim Makame  Khamis Makame katika Khutba yake ameeleza kuwa ni jukumu la kila Muislamu kuungana na Serikali katika kuijenga Zanzibar yenye Maendeleo kwa Nia ya kutafuta Radhi za Allah.

Aidha Maalim Makame ameeleza kuwa umefika wakati Viongozi wakuu kuvumilivu na kuwafahamisha wanaokejeli na kudharau mema yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusema kuwa hiyo ni Neema kutoka kwa Allah Mtukufu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.