Habari za Punde

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA IMEX NCHINI UJERUMANI

 

Eng. Abdullah Al-Jadi (Kulia) kutoka Kuwait akishuhudia Mgeni kutoka Saudi Arabia akivalishwa shuka la kimasai katika banda la Tanzania.

Afisa Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Maria Lazaro akiwa katika mazungumzo na wageni kutoka nchi za Saudia Rabia na Kuweit waliotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya IMEX.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki katika maonesho ya ”Worldwide Exhibition for Incentive Travel, Meetings, and Events (IMEX) yaliyofanyika katika mji wa Frankfrut nchini Ujerumani kuanzia tarehe 31 May, 2022 mpaka tarehe 2 Juni, 2022.

Maonesho ya IMEX ni mahsusi kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Mikutano na Matukio ambayo hufanyika kila mwaka nchini Ujerumani. Nchi mbalimbali duniani zinatumia maonesho haya kwa ajili ya kutafuta fursa za kuandaa mikutano na matukio ya kimataifa katika nchi zao.

“Ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya umetoa fursa kwa waandaaji wa mikutano mikubwa na matukio ya kimataifa kutoka nchi mbalimbali  kuonyesha nia ya kuleta mikutano hiyo kufanyika nchini Tanzania. Baadhi ya wageni waliotembelea banda la Tanzania wanatoka nchi za Marekani, Saudia Arabia na Kuwait na wameahidi kuleta makundi ya watali kuja nchini Tanzania”.

Hayo yalisemwa na Afisa Utalii wa TTB, Bi. Maria Lazaro wakati wa maonesho yanayoendelea nchini Ujerumani, na kuongeza kuwa “Bodi ya Utalii Tanzania inatumia Onesho la IMEX kutangaza fursa za uwekezaji katika kumbi za mikutano, malazi na usafiri wa anga.

Bodi ya Utalii Tanzania inaendelea na juhudi za kupata uanachama katika vyama vinavyohusiana na  uandaaji wa mikutano ya kimataifa ili kuweza kutanua wigo wa kupata fursa ya kuleta mikutano mikubwa ya kimataifa nchini Tanzania

 

CAPTION:

1: Afisa Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Maria Lazaro akiwa katika mazungumzo na wageni kutoka nchi za Saudia Rabia na Kuweit waliotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya IMEX.

 

2: Eng. Abdullah Al-Jadi (Kulia) kutoka Kuwait akishuhudia Mgeni kutoka Saudi Arabia akivalishwa shuka la kimasai katika banda la Tanzania.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.