
Mheshimiwa
Hussein Bashe Waziri waKilimo akizungumza wakati akifungua semina ya
siku mbili iliyowahusisha wadau wa Sekta ya Umwagiliaji mjini Morogoro

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bw, Raymond Mndolwa akizungumza wakati wa semina hiyo.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe mbalimbali walioudhuria Semina hiyo Walioketi. Katikati ni Waziri waKilimo Mheshimiwa Hussein Bashe.Na.Mwandishi Wetu - MOROGORO
Waziri wa
Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe, amesema kwa Mwaka wafedha ujao Wizara
yake itatumia Shilingi Bilioni 420 katika ujenzi wa Miundo mbinu ya
Skimu za umwagiliaji ikiwemo Hekta elfu kumi kwa ajili ya uzalishaji wa
Mbegu ambapo wadau wa sekta binafsi watapewa kipaumbele kwa ajili ya
kuzalisha Mbegu, ujenzi wa mabwawa 14 yatakayokuwa na miundombinu ya
umwagiliaji kwa matumizi ya kilimo na mifugo.
Aliyasema hayo
leo Mjini Morogoro wakati akifungua semina ya siku mbili iliyowahusisha
wadau wa Sekta ya Umwagiliaji mjini Morogoro, Waziri Bashe ameendelea
kusema kuwa utekelezaji wa kazi hiyo utakwenda sambamba na kuanzishwa
kwa Ofisi za Umwagiliaji za Wilaya nchi nzima pamoja nakuajiri
wasimamizi wa Skimu za umwagiliaji watakaohusika kusimamia zoezi la
ukusanyaji wa ada na tozo za umwagiliaji kwa uhakika.
Eneo
lingine la kipaumbele kwa Waziri Bashe ni pamoja na kuwasaidia Wakulima
Wadogowadogo kupataTeknolojia bora za kilimo cha umwagiliaji kwa bei
nafuu ili waweze kupata tija na kuchangia ongezeko la mavuno katika
sekta ya umwagiliaji, zoezi hilo litawahusu pia Vijana
wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.
Kwaupande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw,Raymond Mndolwa
amewataka watumishi wote wa tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya kazi
kwa bidi na ubunifu ili kutimiza matarajio yaliyowekwa na serikali,
akiamini taasisi yake inauwezo wakutekeleza majukumu yaliyopangwa na
serikali kwa wakati, ufanisi na ubora unaotakiwa katika kuhudumia
wananchi.
“ Nitamsapoti kila mtumishi aweze kutimi za wajibu wake, tumejipanga na lililopo mbele yetu tunaweza kulitekeleza”
Semina
hiyo ya siku mbili imewashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo sekta
binafsi, Wakulima wadogo, Wataalam waBenki, Vyama vya Ushirika,
Wahandisi na Maafisa kilimo wa Wilaya ikiangazia namna ya kuboresha
maeneo matatu muhimu katika kilimo cha umwagiliaji ,uzalishaji, huduma
za u mwagiliaji na njia bora yakukusanya Ada naTozozaUmwagiliaji.
No comments:
Post a Comment