Habari za Punde

DC Kiswaga Atumia Mchezo wa Bao Kuhamasisha Wananchi Kujitokeza Kuhesabiwa Siku ya Sensa.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiongea na wananchi kuhusu umuhimu wa SENSA ya watu na makazi kwa wananchi wa Tarafa ya Pawaga.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WANANCHI wa wilaya ya Iringa wametakiwa kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA ili kutengeneza taswira halisi ya serikali kujua idadi ya wananchi kwa lengo la kutafuta namna bora ya kuwapelekea maendeleo wananchi kulingana na idadi iliyopo kila eneo.

Akizungumza wakati wa sikuku za sabasaba mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga alisema kuwa wananchi watakiwa kujitokeza siku SENSA ili waweze kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo yao.

Kiswaga aliwata viongozi mbalimbali kutumia fursa ya uwepo wa michezo kwenye vijiji,mitaa,kata na tarafa kuhamasisha wananchi wajitokeze kuhesabiwa.

Alisema kuwa kwenye kila mchezo kunakuwa nakundi kubwa la wananchi hivyo ni rahisi sana kufikisha ujumbe wa SENSA na ujumbe ukapokelewa vizuri.

Kiswaga alisema kuwa mchezo wa Bao la solo limekuwa kiunganishi kikubwa kwa wananchi na serikali kama ambavyo hayati mwalimu Nyerere alitumia mchezo huo katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika na kufaulu kuupata uhuru huo.

Hivyo michezo yote inatakiwa kupewa kipaumbele sawa ili kuiweka jamii ya wanamichezo pamoja na kutumia fursa za michezo kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Iringa vijijini,Makala Mapesa alisema kuwa mchezo wa bao la solo ni mchezo ambao unachezwa na watu wa lika zote kwa ajili ya fursa na kutengeneza fursa za kimaendeleo wakiwa wanacheza mchezo huo.

Mapessa alisema kuwa mchezo wa bao la solo umekuwa moja ya michezo ambayo unatakiwa kutumia akiri nyingi na maarifa kuliko kutumia nguvu hivyo ukicheza mara kwa mara mchezo huo akili yako itachangamka kwenye kufikiri.

Aliowamba vijana kuucheza na kuenzi mchezo huo wa kitamaduni kwa kuondoa dhana ya kuwa mchezo huo ni wawazee tu na sio mchezo wa vijana.


Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akikabidhi zawadi kwa mshindi wa mchezo wa bao na kuongea na  wananchi kuhusu umuhimu wa SENSA ya watu na makazi kwa wananchi wa Tarafa ya Pawaga
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kucheza mchezo wa bao mbele ya mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga juu ya umuhimu wa SENSA ya watu na makazi
Baadhi ya wananchi waliojitkeza kumsikiliza mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga juu ya umuhimu wa SENSA ya watu na makazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.