Habari za Punde

Waziri Mhe.Simbachaweni Aongoza Kikao cha Mawaziri Dodoma.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene (kushoto) akiongoza Kikao cha Kutatua mgogoro wa ardhi Rutoro na Mwisa II, Kagera kilichohusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, wawakilishi na wataalamu (kulia) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. John Jingu katika Ukumbi wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene (kushoto) akiongoza Kikao cha Kutatua mgogoro wa ardhi Rutoro na Mwisa II, Kagera kilichohusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, wawakilishi na wataalamu (kulia) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. John Jingu katika Ukumbi wa ofisi hiyo Juni 30, 2022 Jijini Dodoma.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

 Na Mwandishi wetu- Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameongoza kikao cha Kutatua Mgogoro wa Ardhi Rutoro na Mwisa II mkoani Kagera ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuishi kwa amani na kufanya shughuli  zao  kwa kuzingatia sheria.

Kikao hicho kimefanyika Juni 30, 2022 Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kikihusisha Mawaziri , Makatibu Wakuu, wawakilishi na wataalamu ambapo miongoni mwa Mawaziri waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa  na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba  Ndaki.

Mhe. Simbachawene alisema suala la migogoro ya ardhi linapaswa kutafutiwa ufumbuzi haraka pindi linapojitokeza kwani husababisha madhara makubwa kama watu kupoteza , mali kuharibiwa na uharibifu wa miundo mbinu.

Aidha alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu kwa wananchi wake kuhakikisha shughuli zote za kilimo, ufugaji na nyanja nzima ya uwekezaji zinafanyika katika mazingira sahihi  na salama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.