Habari za Punde

Kamati Ya Ustawi wa Jamii Yaitaka SUZA Kuzalisha Wataalamu wa Uchumi wa Buluu


Kamati Ya Ustawi Wa Jamii Ya Baraza La Wawakilishi Imesisitiza HAJA KWA Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar SUZA kuweka kipaombele katika kuzalisha wahitimu wenye sifa ambao watakua mchango mkubwa katika kutekeleza dhana ya uchumi wa buluu.

Wajumbe wa kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Mhe Mohammed Ahmada Salum wametoa ushauri huo wakati walipokutana na viongozi wa chuo hicho huko katika makao makuu yake Tunguu.

Wamesema chuo hicho kina wajibu wa  kuwaandaa vijana ili waweze kupata stadi na ujuzi stahiki kwa nia ya kuelekea katika uchumi wa buluu unaotokana na dhamira ya serikali ya awamu ya nane chini ya dkt hussein mwinyi ambapo serikali haitegemei wataalamu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutekeleza dhamira hiyo wakati vipo vyuo vinavyozalisha wahitimu kila mwaka.

Mapema Afisa Dhamana Wa Chuo Kikuu Suza Kisiwani Pemba Said Khamis Faki na viongozi wengine wa chuo hicho wameelezea mafanikio waliyoyapata ikiwemo kuzalisha wataalamu wa sayansi ambao wengi wao wameajiriwa serikalini na sekta binafsi na  kupelekea kupunguza pengo la walimu wa kada hiyo lilioko maskulini.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.