Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amtembelea Mwanasia Mkonge Mzee Ali Ameir Mohammed Nyumbani Kwake Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mzee Ali Ameir Mohammed alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa kumsalimia na kumtembelea na kumjulia hali yake.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mzee Ali Ameir Mohammed, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Donge, Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja kumjulia hali yake leo 7-8-2022 na (kushoto kwa Mzee Ali ) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mzee Ali Ameir Mohammed alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja kumtembelea na kujua hali yake na (kushoto kwa Rais) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassam Othman Ngwali
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali (kushoto kwa Rais) ya kumuombea Mzee Ali Ameir Mohammed (kulia) aliyekuwa Mbunge wa Donge, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzani na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani, kumtembelea na kumjulia hali yake.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu na Mzee Ali Ameir Mohammed, kinachozungumzia historia ya Vyama vha TANU na ASP, kabla ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi,kitabu hicho ameandika yeye kwa ajili ya historia ya Vizazi vijavyo, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Donge Kichavyani Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.