Habari za Punde

Shaka - Sensa Haina Nasaba Bali Imebeba Maslahi ya Taifa

 

KATIBU wa NEC Itakadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi  Ndg. Shaka Hamdu amesema Sensa ya Watu na Makazi haina nasaba bali imebeba maslahi ya taifa, kwakuwa maendeleo hayachagui hivyo katika tukio hilo viongozi wote na vyama vya siasa wameungana na kuongea kauli moja.

Amesisitiza katika tukio hilo vyama zaidi ya 13 vimetoa tamko la kuhimiza na kuhamasisha umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi hivyo jamii ni muda sahihi wa kuhesabiwa ili kuiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo.

Akizungumza leo nyumbani kwake Mjini Unguja Shaka alisema haina nasaba bali imebeba maslahi ya taifa, kwakuwa maendeleo hayachagui na viongozi wameungana huku vyama zaidi ya 13 vikitoa tamko ya kuhimiza na kuhamasisha umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi.

Alisema, taifa limeingia historia nyingine kwa kufanyika kwa Sensa ya sita,tukio ambalo ni muhimu kwa mustakbari wa maendeleo.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani zilizokutana na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, jamii na siasa yenye mafanikio na changamoto hivyo Sensa ilikuwa  inahitajika kwakuwa ni muhimu.

“CCM tunaipongeza serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kwa kutenga fedha, kusimamia na  kuhakikisha jambo hilo linatekelezeka, hivyo Rais Samia ni mkombozi aliyehakikisha jambo hili nyeti linafanyika kwa mafanikio makubwa ya taifa,”alisema.

Shaka alieleza kuwa,Sensa ya sasa na ya mwaka 2012, ya sasa imekuwa na muamko mkubwa na Watanzania wengi wamejitokeza huku hamasa ikiwa ya kutosha hususani katika mitandao ya kijamii hivyo wanatarajia  itafanikiwa.

“Pia maboresho yaliyofanyika tulizoea anakuja kalani na mnatumia saa 2 kujaza dodoso  lakini kwa sasa dunia imebadilika na nyakati na muda tulionao Tanzania tupo kwenye mfumo wa mabadiliko ya TEHAMA tunafanya sensa hii kwenye mifumo hiyo na faida tumeiona,”alisema. #sensabika #sensa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.