Habari za Punde

Waziri Simbachawene amshukuru Rais kwa fedha ya miradi maendeleo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (Kulia) akiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipata juice katika banda la lishe Halmashauri ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Bwn. Sahili Geraruma akikagua barabara ya lami Km 1  Mpwapwa mjini kabla ya kuizindua.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha billioni 16 kwa mwaka uliopita wa fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mpwapwa.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. George Simbachawene katika mapokezi ya mbio za mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.  Wenye kauli Mbiu “sensa ni Msingi wa Mpango wa maendeleo. Shiriki kuhesabiwa  tuyafikie maendeleo ya Taifa.”

“Watu wanahitaji kusikia shida zao zinazungumzwa, ni imani yangu kwamba viongozi tutaendelea kushirikiana na fedha yoyote ya mradi wa maendeleo itakayokuja tutaitumia vizuri”

Waziri Simbachawene amepongeza timu ya wakimbiza Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kufanya kazi nzuri. Mwenge wa uhuru umekimbizwa kwa umbali wa km 100 na umezindua miradi miwili, miradi mingine miwili imewekwa jiwe la msingi na mradi mmoja kutembelewa yenye thamani ya zaidi billion 1.4.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.