Habari za Punde

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LA KUTANA NA UONGOZI WA WAKALA WA KUUZA VIFAA VYA ZIMAMOTO (FIRE DEALER) JIJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Mawakala wa kuuza na kusambaza vifaa vya zimamoto na uokoaji (TAFEDA) Bwa. Hamis Balowa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema

Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Viongozi wa Chama cha TAFEDA, wakifatilia kikao kilichofanyika mapema leo tarehe 2 Septemba, 2022 Makao Makuu ya Jeshi hilo. (PICHA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI)

Mapema leo Septemba 02, 2022, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekutana na Uongozi wa wauzaji na wasambazaji wa Vifaa vya kuzimia moto “Fire Dealer” kupitia chama chao cha TAFEDA na kujadili mambo mbalimbali kuhusu Moto na Maokozi zikiwemo changamoto zinazo wakabili katika utendaji wao.

Akiwasilisha changamoto hizo kwa kamishna Jenerali, Mwenyekiti wa TAFEDA Hamisi Balowa amesema wanakabiliwa na ukosefu wa Wataalamu wenye ujuzi wa elimu ya sayansi ya Moto na Maokozi kwa sababu gharama za kulipia masomo hayo yanayotolewa na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji ziko juu sana.

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, amewahakikishia Viongozi hao kuzifanyia kazi changamoto hizo kama ambavyo serikali imefanikiwa kuwashushia Tozo ya uwakala wa uuzaji na usambazaji wa vifaa vya kuzimia moto.


“Ninyi ni sehemu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu kazi mnazozifanya mnasaidia kuimarisha Usalama wa Watu na Mali zao pamoja na Kuokoa Maisha”. Alisema CGF Masunga.

 

Aidha Kamishna Jenerali Masunga, amewahaidi kuzitatua changamoto zao na kuwataka wajitangaze kwani jamii haijui uwepo wao pamoja na huduma wanazozitoa, kwani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji halijihusishi na uuzaji na usambazaji wa bidhaa hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.