Habari za Punde

Kamisaa wa Sensa akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 06 Septemba 2022 Jijini Dodoma.
Amesema kiwango cha kaya zikizohesabiwa nchi nzima limefikia asilimia 99.99 na limehitimishwa rasmi.
Kwa upande wa Sensa ya Majengo, asilimia 99.87 ya majengo yote nchini yamehesabiwa na taarifa zimekusanywa na kati ya majengo hayo asilimia 100 ya majengo yote yaliyochukuliwa taarifa zake yanehakikiwa anwani za makazi.Aidha amesema matokeo hayo yatatolewa mwezi Octoba  2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.