Habari za Punde

MAFAO TEGEMEO LA MWISHO KWA MSTAAFU

 
Na.Adeladius Makwega-WUSM

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Bi Zahara Guga amesema watumshi wa umma waadilifu hawana kingine wanachokitegemea zaidi ya pesa zao za mafao ya kustaafau, hivyo ameishauri PSSSF kuwalipa watumishi wa umma haki yao hiyo kwa wakati na kama malipo ya mkupuo yanachelewa basi malipo ya kila mwezi yaanze kulipwe mara baada ya kustaafu wakati mahesabu mengine yanafanyika.

Haya yamesemwa katika semina maalumu iliyotolewa na PSSSF Septemba 2, 2022 kwa watumishi wizara hii Mtumba Mji wa Serikali Jijini Dodoma.

“Mtumishi anategemea mshahara, posho na marupurupu mengine akiwa kazini, sasa kazi imekwisha, hana chochote cha kutegemea, kuna watumishi wanatumia miaka mitatu kweli? Mpaka leo hajalipwa, mwingine anatembea hadi anapatwa na mangonjwa, kama tumeamua tunakwenda katika asilimia 33, basi wastaafu walipwe kwa wakati.”

Naye Bi Neema Said Ramadhani ambaye ni Afisa Rasilimali watu Daraja la Pili wizarani hapa aliuliza, “Baadhi ya watumishi kuchangia mifuko miwili huku jambo hilo likiwa na changamoto wakati wa malipo ya mwisho, je malipo yatakuwaje?”

Akiyajibu maswali hayo Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati Hajji Khamisi alisema kuwa mfumo wa malipo kwa wanachama waliochangia mifuko miwili, kila mfuko utalipa kwa mujibu wa kanuni huku muda wa uchangiaji wake utajumilishwa kuona kama mtumishi huyo ana haki ya kulipwa mafao ya mkupuo au la.

Meneja Khamisi alimalizia kwa kutaja faida kadhaa ya ukokotoaji wa sasa, kwani hauwabagui wafanyakazi wa umma na wale wa taasisi binafsi na ndani ya mfuko huo kila mstaafu ana nafasi ya kuyakuta mafao yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.