Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein Ameongoza Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar Tarehe 4-9-2022

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja kuongoza Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Afisi Kuu Kisiwandui Jijini Zanzibar.
Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakisoma makabrasha ya Kikao kabla ya kuaza kwa kikoa hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein.

Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakisoma makabrasha ya Kikao kabla ya kuaza kwa kikoa hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja leo kuongoza Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Sadala Mabodi
WAJUMBE wa Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja wakati Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein kuwasili katika ukumbi kwa ajili ya kuongoza Kikao hicho kilichofanyika leo 4-9-2022
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dkt. Abdalla Sadala Mabodi akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, kuongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja leo 4-9-2022
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo 4-9-2022 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja na (kulia ) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe Hemed Suleiman Abdulla
WAJUMBE wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) akiongoza Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja leo 4-9-2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.