Habari za Punde

DC Moyo Aamuru Kuondolewa kwa Mipaka ya Ardhi Inayosababisha Migogoro

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Mkumbwanyi.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ameamuru kuondolewa kwa alama za mipaka ya Kijiji cha Mkumbwanyi, Kisanga na Makuka iliyowekwa hivi karibuni baada ya kupokea malalamiko kuwa alama hizo ziliwekwa kimakosa na kusababisha Migogoro ya baina ya vijiji hivyo

 

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkumbwanyi, Mkuu wa wilaya ya Iringa alisema kuwa baada ya kusikiliza malalamiko ya Wananchi wa Kijiji Cha Mkumbwani amejiridhisha kuwa alama hizo za mipaka zimewekwa pasipo kushirikisha pande zote za Serikali za vijiji jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

 

Moyo amefafanua kuwa kwa mujibu wa taratibu unapotaka kuweka alama za mipaka baina ya kijiji na Kijiji lazima ushirikishe pale zote na ziridhie ni wapi Mpaka uwekwe ili kuepusha Migogoro inayoweza kuhatarisha usalama wa Wananchi wa vijiji husika.

 

Awali kupitia taarifa iliyowasilishwa katika Mkutano huo wa hadhara ilielezwa kuwa Maafisa wa Ardhi kutoka Wizarani walifika Kijijini hapo Kwa lengo la kushughulikia mgogoro wa mipaka Lakini kabla ya muafaka kamili waliweka alama hizo jambo lililotajwa kuwa batili na lilolochochoa uhasama baina ya pande zinazopingana.

 

Licha kuamuriwa alama hizo kuondolewa Kiongozi huyo wa Wilaya ya Iringa amemuagiza Kaimu Afisa Tarafa kupeleka taarifa ya kusitishwa Kwa shughuli zote Katika maeneo yenye mgogoro wa mipakahuku akiliamuru Jeshi la Polisi kumkamata yeyote atakayekwenda kinyume na Amri hiyo 

 

Alisema kwenye kushughulikia utatuzi wa Mgogoro huo Serikali ya wilaya kupitia kamati ya Ulinzi na Usalama haitosita kuchukua hatua Kwa Mtu yeyote wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa kikiwemo Chama Cha Mapinduzi watakajihusishakukaidi Amri hiyo wakati hatua za utatuzi zikiendelea kufanywa na kamati hiyo

 

Afisa ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Geoffrey Kalua alisema kuwa kitendo cha Wataalam kutoka Wizarani kuweka mipaka pasipo kushirikisha pande zote ni kinyume cha taratibu hivyo maamuzi ya kuondoshwa kwa alama hizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya Iringa Mohamedi Hassani Moyo ni maamuzi sahihi kisheria.  

 

Kwa upande wake Kaimu Afisa Tarafa ya Pawaga Emmanuel Ngabuji ameahidi kutekeleza agizo la kuondoa alama hizo kwakushirikiana na Afisa Tarafa ya Isimani kama walivyoagizwa Huku Jeshi la Polisi wilaya ya Iringa kupitia Mkuu wa Polisi wilaya akiahidi kuimarisha Ulinzi wakati wa uondolewaji wa mawe ya alama za mipaka.

 

Awali akimueleza mkuu wa wilaya na afisa ardhi Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Diwani wa kata ya Mboliboli Yusuf Msamba alisema kuwa toka zimewekwa alama hizo zimezua hali ya sintofahamu kwa wananchi wa Kijiji cha Mkumbwanyi hivyo anauomba uongozi huo kutatua mgogoro huo ili kurudisha amani iliyopotea kwa wananchi wote wa Kijiji hicho.

 

Msamba alisema kuwa maafisa ardhi kutoka wizarani waliweka alama za mipaka ya Vijiji bila kushirikisha pande zote mbili hivyo hilo lilikuja jambo ambalo ni kinyume cha sheria za ardhi na zimesababisha kuibuka kwa mgogoro mpya ambao haukuwepi awali.Kaimu Afisa Tarafa ya Pawaga Bw.Emmanuel Ngabuji akimuelezea mkuu wa wilaya historia ya mipaka ya kijiji cha Mkumbwanyi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.