Habari za Punde

Kufanyika kwa Vikao vya Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Ngazi ya Taifa

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwataarifu wanachama wake na watanzania wote kuhusu kufanyika kwa vikao vya kawaida vya uongozi ngazi ya Taifa Jijini Dodoma kuanzia tarehe 28 Oktoba, 2022 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (CC) na tarehe 29 Oktoba, 2022 Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC).

Pamoja na mambo mengine vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama walioomba uongozi katika ngazi ya mikoa na taifa kwa upande wa jumuiya pamoja na chama.

Vikao hivyo vimetanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kilichofanyika tarehe 24 na 25 Oktoba, 2022 Jijini Dodoma.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI.
27 Oktoba, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.