Habari za Punde

Shujaa Majaliwa tayari ameshapokelewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

 

  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI 

Simuyamaandishi: “ZIMAMOTO KUU” SimuNambari: 255-26-23200243 Telefax: 255-26-23200243 BaruaPepe: fire.rescue@frf.go.tz Tovuti: www.frf.go.tz 

DODOMA  07 Novemba, 2022 

Ofisi ya Kamishna Jenerali Makao Makuu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 

1 Mtaa wa Zimamoto 

S. L. P. 1509 

41102 VIWANDANI, DODOMA

TAARIFA KWA UMMA 

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamishna Jenerali John Masunga, anaujulisha umma kuwa Majaliwa Jackson Samweli, ameshapokelewa na Jeshi la Zimamoto na  Uokoaji. Hivyo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi  Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, tayari yameshatekelezwa. 

Majaliwa anatarajiwa kuanza mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji pamoja na ya Uaskari  katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo Wilaya ya Handeni  Mkoa wa Tanga. 

Ikumbukwe kuwa tarehe 06 Novemba, 2022 ilitokea ajali ya kuanguka kwa Ndege ya Precision Air katika Ziwa Victoria, ajali hii ilisababisha majeruhi na vifo. Majaliwa  alionesha ujasiri wa hali ya juu, kwa kuokoa wahanga 24 wa tukio hilo.  

Kamishna Jenerali anatoa shukrani za dhati kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,  Taasisi za Umma na Binafsi, pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kagera kwa ushirikiano  mkubwa waliotoa katika zoezi la uokoaji katika ajali hiyo. 

Kamishna Jenerali anatoa pole kwa Wafiwa wote na kuwaombea faraja katika kipindi  hiki kigumu wanachopitia, anawatakia majeruhi wote afya njema. 

Anawasihi Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika  kuokoa Maisha ya watu na mali dhidi ya majanga mbalimbali, 

Imetolewa na; 

SACF - Puyo Nzalayaimisi 

Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 

Makao Makuu Dodoma 

07 Novemba, 2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.