Habari za Punde

Viongozi wa Dini Kuwaelimisha zaidi Wananchi hasa wa Vijijini juu ya Malezi ya Watoto kwa Kuzingatia Misingi ya Dini Zao

Na.Maulid Yussuf - Pemba.

Afisa Mdhamin Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw.Hafidh Ameir Shoka, amewataka viongozi wa dini kuwaelimisha zaidi wananchi hasa wa vijijini juu ya malezi ya watoto kwa kuzingatia misingi ya dini zao ili kusaidia kupunguza vitendo vya udhalilishaji kwa watoto.

Amesema hayo wakati akifungua mkutano wa viongozi wa dini juu ya uwasilishaji wa utekelezaji wa kazi zao za kipindi cha Oktoba hadi Disemba pamoja na mikakati yao ya kipindi cha Januari hadi machi, katika Ukumbi wa Samail Hoteli Gombani Pemba.

Amesema ni jambo linalotia aibu kwa Zanzibar ambayo watu wake asilimia kubwa wapo katika misingi ya kidini lakini vitendo vya  udhalilishaji kila kukicha vimekuwa vikiripotiwa.

Amesema ni lazima kuongeza nguvu kwenye  mapambano hayo kwa kuwahamaisha wazazi na walezi, kuwaelimisha watoto tokea wadogo kwenye hatua za awali za makuzi yao iIi iwe rahisi kuwajenga katika misingi ya imara ya kidini pamoja na kuwa nao karibu kuwaelimisha athari za vitendo vya udhalilishaji  ili kusaidia kupunguza vitendo hivyo nchini. 

Aidha bwana Hafidh, amewasisitiza viongozi hao wa dini kusaidia kurejesha maadili ykiyoambatana na upendo na  huruma ambayo kwa ssa yametoweka yanayochangia kasi ya  udhalilishaji wa kijinsia.

Hata hivyo amewanasihi kuishajiisha jamii kujitokeza katika kutoa ushahidi wakati watakapohitajika, kwani kesi nyingi zimekuwa zikifutwa kwa kukosa ushahidi na kupelekea waathiwa wa vitendo hivyo kukosa haki zao.

Kwa upande wao viongozi wa dini wamesema pamoja na mafanikio wanayoyapata katika utoaji wa Elimu juu ya masuala mazima ya udhalilishaji lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowafanya kukosa ufanisi mzuri wa kazi zao.

Wamezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na kukosa malipo ya vikao vyao vitatu vilivyopita pamoja na posho zao za kila baada ya miezi mitatu.

Mkutano huo umewashirikisha vIongozi wa dini kutoka Wilaya ya Micheweni, Chakechake, Wete na Mkoani.

MWISHO 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA UHUSIANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.