Habari za Punde

Wazazi na Walezi Nchini watakiwa kushirikiana katika Malezi ya pamoja


 Wazazi na Walezi Nchini wametakiwa kushirikiana katika Malezi ya pamoja ili kupata kizazi chenye Maadili Mema.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo wakati akiwasalimia Waumini wa Masjid Salummaka Miti Ulaya alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 Amesema Zanzibar ilisifika kwa Mila na Desturi njema zilizojengeka kwa  Jamii kulea Watoto kwa pamoja ambapo jamii ya sasa imekosa malezi hayo hatua ambayo inapelekea kupata kizazi kilichokosa maadili.

 Aidha amesema  Uislamu umeelekeza namna ya kulea watoto kupitia kitabu kitukufu cha Qur-ani pamoja na Hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) jambo ambalo jamii ya wazanzibari ikikishika Kitabu hicho itaweza kupata Kizazi kitakachoshika Qur-ani.

 Alhajj Hemed ameongeza kuwa miongoni mwa jukumu la wazazi ni kulea watoto na kuwakuza katika makuzi mema jukumu ambalo siku ya Kiama kila mzazi ataulizwa na Allah Mtukufu namna alivyolea watoto wake.

Ameongeza kuwa Jamii kubwa ya Wazanzibari imepotea katika maadili hatua ambayo inapelekea kupata makundi yanayoendeleza vitendo viovu ikiwemo Ubakaji, Wizi, udhalilishaji na vyenginevyo.

 Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka waumini hao kuwa na lugha nzuri baina yao katika kuhimiza juu ya suala la kufanya Ibada na kuwataka Waumini kwa ujumla kuwasaidia Masheikh katika kuhimizana juu ya suala la kufanya Ibada.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha Amani iliyopo ili kutoa Fursa kwa Serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 Akitoa Khutba katika Sala hiyo Sheikh Fadhil Abdallah Idarous amewataka Waumini hao kurudisha heshima ya Zanzibar iliyosifika kwa kuwepo kwa wanazuoni wakubwa walioshika Dini ambao walipelekea kurithisha kizazi Chao suala la Uchamungu.

 Aidha Sheikh Fadhil amewakumbusha wafanyabiashara kuzingatia nidhamu zilizoelezwa katika Qur-ani namna ya kufanya biashara

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.