Habari za Punde

Karne Hii ya 21 ni ya Sayansi na Teknolojia -Waziri Pembe

Na Maulid Yussuf WMJJWW

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajua umuhimu wa Sayansi na mchango wake Katika Karne hii ya 21 ni ya sayansi na  teklojia.

Amesema hayo wakati akifungua maabara ya sayansi ya Skuli ya Sekondari ya Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. 

Amesema  ujenzi wa maabara za sayansi utasaidia Taifa kuzalisha wataalam wazalendo ambao wanaendana na mabadiliko ya sayansi na teklojia.

Amesema katika kupunguza changamoto ya ukosefu wa maabara Wizara ya Elimu Zanzibar imejenga  maabara 10 Unguja na Pemba ikiwemo ya Fukuchani.

Pia amesema uwepo wa maabara hiyo utachochea kuamsha ari kwa Wanafunzi kusoma kwa bidii na kupelekea kupata matokeo mazuri katika mitihani ya Taifa.

Amesema Serikali ya awamu ya nane  imeamua kuimarisha ubora wa Elimu  ili kuleta Mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Mapema Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgullam Hussein amesema ili kuyaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Wizara itaendea kuboresha sekta ya Elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu mbalimbali ili Wanafunzi waweze kusoma  kwa vitendo.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Ayoub Mohamed amesema ni jambo la busara kuboresha sekta ya Elimu kwani ni sekta mama katika ukuzaji wa Uchumi wa Taifa.

Amesema ujenzi wa maabara hiyo utasaidia kuinua kiwango Cha ufaulu wa Wanafunzi kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akisoma taarifa ya kitaalam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Dkt Mwanakhamis Adam Ameir   amesema Jumla ya shillingi million 400  zimetumika kwa ajili ya ujenzi huo wa  vyumba vitatu vya maabara za kisayasi chini ya ufadhili wa Shirika la Koika.

Amesema lengo la ujenzi wa maabara hiyo ni kuhakikisha Wanafunzi wanasoma kwa vitendo na kutimiza Mikakati ya malengo ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.

mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.