Na Shamimu Nyaki
Naibu Waziri wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul Januari 23, 2023 Ofisini kwake Mtumba Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya
viongozi wa Shirikisho la Filamu Nchini.
Katika kikao hicho Naibu
Waziri Gekul, amepokea changamoto na mapendekezo kuhusu namna bora ya kuboresha
uendeshaji na utendaji wa Shirikisho na Vyama vinavyounda Shirikisho hilo.
Mhe. Gekul, ameelekeza Bodi
ya Filamu na Baraza la Sanaa la Taifa kupitia upya Katiba ya Shirikisho hilo
pamoja na Vyama vyote ili kuangalia mapungufu na kuyafanyia kazi.
Aidha ameagiza Bodi ya
Filamu pamoja na BASATA kukutana na viongozi wa Shirikisho na Vyama hivyo kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi
wa Shirikisho na Vyama vyake.
No comments:
Post a Comment