Habari za Punde

Uhusiano wa China na Zanzibar ni wa Kupigiwa Mfano

Na. Maulid Yussuf WMJJWW Zanzibar.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma amesifu ushirikiano uliopo kati ya Zanzibar na China kuwa ni wa kupigiwa mfano.

Mhe Riziki amesema hayo katika hafla ya kusherehekea
Mwaka mpya wa Kichina iliyoandaliwa na Jumuiya ya vijana wa China  inayojitolea katika kuchangia Afrika, SINO AFRICA YOUTH (SAY)  ya hapa Zanzibar ambayo imeanzishwa na Bi. Li Yaya kutoka China, huko Tomondo Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana nao pamoja na wadau wengine na wadau wengine ili kuleta maendeleo nchini. 

Mhe Riziki amesema uamuzi alioufanya Bi. Li wa kuamua kusherehekea mwaka mpya wa nchi yake kwa kupika Chakula cha mchana kwa ajili ya kuwalisha watoto waliopo nyumba ya kulelea watoto Mazizi, Wazee wanaoishi katika makao ya wazee Sebleni na Welezo, ni uamuzi mzuri na wa kupongezwa.

Hivyo ametumia nafasi hio kuishukuru Jumuiya hiyo sana kwa uamuzi huo ambapo amewaomba Jumuiya na Taasisi nyengine kuwa Wizara milango yake  ipo wazi  kwa yeyote atakaetaka kuchangia kwa ajili ya wazee au watoto  kwani ni sehemu pia ya sadaka kwao.

Nae Muanzilishi wa Jumuiya ya vijana wa China  inayojitolea katika kuchangia Afrika, SINO AFRICA YOUTH (SAY), Bibi Li Yaya amesema Wameandaa chakula kwa ajili ya watoto pamoja na wazee ikiwa ni sadaka yao katika kusherehekea mwaka mpya wa nchi yao.

Amesema wanaendelea katika kuwafundisha vijana mbalimbali lugha ya kichina ili iwasaidie katika kujiajiri wao wenyewe ambapo mpaka sasa wameshafundisha wanafuzi 288 wakiwemo wakiwemo Walimu.

Hata hivyo bibi Li,  ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano wanaoupata hasa katika  Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa kupokea sadaka zake kwa ustawi wa Umma.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwashuku wazanzibari kwa kuendelea kumpa ushirikiano pampja na amani na upendo ambao umemfanya kujihisi kama yupo na familia yake.

Pia amewashukuru wananchi waliofika  kushirikiana nae kwa pamoja katika kusherehekea siku hiyo ya mwaka mpya wa kichina.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.