Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi afanya ziara ya kushtukiza Marikiti Kuu Darajani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mfanyabiashara wa bidhaa za vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja.Bw.Seif Khamis Ali, alipofanya ziara ya kustukiza leo 18-2-2023 na katika marikiti kuu darajani na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia mchele wa Mbeya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-2-2023,na kuzungumza na Mfayabishara wa Bidhaa za Vyakula katika marikiti hiyo  Bw.Seif Khamis Ali na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kusalimiana na Watalii wakitembelea Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kutembelea Wafanyabishara ya vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Unguja leo 18-2-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Mfanyabishara wa Nyama ya Ng’ombe katika Soko la Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-2-2023, wakati  alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti hiyo kuangalia hali ya bidhaa ya vyakula.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akilipia Nyama ya Ng’ombe baada ya kuinunua kwa Bw.Ali Hashim mmoja wa Wafanyabiashara katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo 18-2-2023, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)    
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.