Habari za Punde

Ujumbe wa CPC Watembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed akimkabidhi zawadi ya karafuu (kulia),Balozi wa China Tanzania Bi.Chen Mingijian (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed akimkabidhi zawadi ya karafuu (kulia),Balozi wa China Tanzania Bi.Chen Mingijian (kushoto).
UJUMBE wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed wakiwa katika eneo la historia ya watumwa katika Kanisa la Angilikana Mkunazini Zanzibar.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kuwa serikali ya China imekubali kuwekeza katika miradi mbalimbali inayobeba dhana ya uchumi wa bluu.

Hayo ameyasema Naib Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed 'Dimwa' wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamili ziara ya ujumbe wa Chama Cha Kikomunisti cha Chini visiwani Zanzibar.

Alisema  Serikali ya China imekubali kuwekeza katika bahari hasa katika mazao ya baharini ikiwemo mwani,uvuvi na ufugaji wa kaa.

Alisema mbali na kuwekeza katika miradi hiyo pia wamekubaliana kuwekeza ktika miradi ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar kwa kujenga nyumba za watumishi zitakazouzwa kwa gharama nafuu ili viongozi,watumishi na watendaji wa CCM wapate makaazi bora ya kuishi.

''Ziara hii imekuwa na mafanikio makubwa kwani tumejadili mambo mengi ya msingi yanayolenga kutatua kero za wananchi na wanachama wa CCM kwa ujumla''.alisema Dkt.Dimwa.

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, alisema CCM inawakaribisha wawekezaji wa ndani ili waweze kuwekeza huku ikifungua milango kwa wawekezaji wa kimataifa.

 Naye Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Khadija Ali Salum amesema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha Uhusiano katika nyanja za utamaduni,Siasa,diplomasia,Uchumi,jamii,michezo na burudani na  uwekezaji.

Alieleza kuwa kwa miaka mingi Chama Cha kikommunist Cha China(CPC) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekuwa ni vyama vyenye urafiki na undugu wa kihistoria katika masuala ya kuimarisha Ilani za Uchaguzi za vyama hivyo.

Alisema ujumbe wa CPC ulipowasili Zanzibar wamevutiwa na mazingira ya Zanzibar na wakaweka wazi nia Yao ya kuja kuwekeza katika sekta ya bahari katika masuala ya usafiri,uvuvi na kilimo cha baharini cha mwani.

Katika maelezo yake Mkuu huyo wa idara ya SUKI Khadija, amesema kuwa CCM inaendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplimasia na Vyama mbalimbali Duniani ili kwenda sambamba na Siasa ya kisayansi inayojikita katika masuala muhimu ya kuondosha changamoto na kero za Wananchi kwa wakati.

Alieleza kuwa Chama Cha CPC,kimekuwa ni nyenzo muhimu katika kuimarisha Serikali za nchi hizi mbili na China imekuwa ikipokea vijana wengi za Tanzania wanaoenda Kwa ajili ya masomo,biashara na utalii.

Khadija,akizungumzia ziara hiyo alisema baada ya ujumbe huo kuwasili Zanzibar majira ya 3:00 asubuhi ulienda katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo na kwa upande wa china ni Naibu Waziri wa idara ya mambo ya nje ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti LiMingxiang.

Baada ya kusaini kitabu walienda kutembelea maeneo ya kihistoria ya jumba la Wananchi katika mtaa wa forodhani na katika soko la watumwa lililopo katika Kanisa la Anglicana Mkunazini Zanzibar.

Mkuu huyo wa Idara ya SUKI,alisema ujumbe huo umekamilisha ziara yake kwa kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.