Habari za Punde

Maskani zitumike kuongeza kipato - Wito


Na Bahati Habibu  

Naibu Waziri Ofisi ya Makamo wa pili Muungano na Mazingira  na Mbunge wa Jimbo la Uzini Khamis Hamza Chilo amewataka vijana kuzitumia maskani kujifunza vitu mbalimbali vitakavyowasaidia kuongeza kipato chao cha kila siku na kuacha kuwa tegemezi.

Kauli hiyo ameitoa huko Mpapa Wilaya ya Kati  wakati wa kukabidhi Television Kwa Vijana wa Maskani ya Bekari iliyopo Mpapa, amesema umefikia wakati kwa Vijana kuzitumia maskani kuboresha hali zao za kiuchumi. 
 
Aidha amewaonya Vijana hao kuacha kuonesha Michezo itakayohamasisha Vijana kujiingiza katika Vitendo viovu ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, ujambazi na matendo mwengine yasiofaa.

"Niwaambie ndugu zangu Leo tumewapaTelevision si kwamba itatuburudisha na kutufunza tu bali pia yaweza kuwa chanzo Kwa Vijana kuharibika Kwa kuiga yasiofaa"  Alisema Waziri Chilo. 

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Haji Shaaban Waziri amewaasa Vijana hao kukemea na kutoa Elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji Kwa lengo la  kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuondosha vitendo hivyo.

Amesema kwa  sasa Zanzibar inakabiliwa na Janga la Udhalilishaji huku takwimu zikionesha asilimia kubwa  ya wafanyaji wa vitendo hivyo ni Vijana.

Aidha amewataka Vijana kudai risiti za ki electronic Kila wanunuapo bidhaa  ili kuzuia upotevu wa mapato ya Serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.