Na Fauzia Mussa Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya Zanzibar kwa kushirikiiana na Pharm Access international imeanzisha mpango maalum wa kuwafikia wagonjwa wa maradhi yasioambukiza katika ngazi ya jamii na kuwapatia elimu pamoja na huduma za Afya.
Hayo yamesemwa na Afisa wa mradi wa wagonjwa wa maradhi yasioambukiza Queen-Ruth Msina wakati alipokua akifanya mahojiano katika zoezi la utoaji wa huduma za Afya kwa ngazi ya jamii lililofanyikaa Koani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema mradi huo ulianzishwa kufuatia uwepo wa changamoto za wagonjwa na madaktari wakati wa utoaji wa huduma za Afya ambao umelenga kutatua changamoto hizo .
Aidha alifahamisha kuwa madaktari wamekua wakielemewa na wingi wa wagonjwa Vituoni jambo linalorejesha nyuma jitihada za kuwahudumia wagonjwa wa maradhi hayo kwa ufanisi kwani muda wa kuwasikiliza huwa hautoshelezi.
Amefafanua kuwa wagonjwa wamekuwa wakitoka masafa marefu na kukaa muda mrefu vituoni kusubiri huduma jambo linawapa ugumu kufuatilia huduma za Afya kwani wengi wao huwa ni wazee wasiojiweza.
Amesema mradi huo unawakutanisha Madaktari na Vikundi vya Wagonjwa wenye maradhi yasioambukiza kwa mwezi mara moja katika Vijiji vyao ambapo wagonjwa hupatiwa elimu na kubadlishana mawazo juu ya maradhi hayo.
"Tumeona wagonjwa wanapata shida kukaa foleni, na wanatoka Masafa marefu jambo linalwarejesha nyuma kurudia tena Kliniki kupatiwa huduma ,mrad huu utawakutanisha wagonjwa na madaktari katika ngazi ya jamii na kuwaweka huru katika kuzungumza changamoto zinazowakabili. " alisema
Mapema Afisa huyo aliishauri jamiii kutokupuza kuhudhuria katika vikao ndani ya shehia zao mara tu wanapotakiwa kufika ili kupata fursa kama hizo kwani zina tija na faida kwao.
Nao wanakikundi cha maradhi yasioambukiza cha Koani wameishukuru Wizara ya Afya kw kushirikiana na Pharm Access kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu na kuahidi kuzifatilia huduma hizo mara tu zinapofika katika jamii.
Jumla ya vikundi 25 vya wagonjwa wenye maradhi yasioambukiza vinatarajiwa kunufaika na Mradi huo Unguja na pemba.
No comments:
Post a Comment