Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Ametoa Sadaka ya Futari Kwa Wananchi wa Kojana Pemba

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi sadaka mmoja wa Mwananchi wa Kojani Pemba, wakati wa ziara ya Siku mbili ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Pemba na kujumuika na Wananchi wa Mikoa Miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba katika Futari Maalum aliyowaandali Wananchi wa Makundi Maalum Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi msaada wa futari Mwananchi wa Kojani Pemba na (kkushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Kojani Pemba baada ya kumaliza kuwakabidhi Sadaka ya Futari, akiwa Pemba kwa ziara ya Siku mbili na kujumuika na Wananchi wa Mikoa miwili ya Kaskazini Pemba na Kusini Pemba katika futari maalum aliyowaandaliwa Wananchi wa Makundi Maalum Pemba.

Wananchi wa Kojani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumaliza kutoa sadaka ya futari kwa Wananchi hao wa makundi maalum Pemba, akiwa katika ziara yake ya siku mbili Pemba.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.