Habari za Punde

Waandishi wa Habari Zanzibar Wapatiwa Mafunzo ya Lishe

Mkuu wa Kitengo cha Lishe Asha Hassan Salmin akizungumza wakati alipokua akiwasilisha  taarifa ya utafiti wa Afya na lishe kwa Waandishi wa Habari,wakati wa mafunzo ya  lishe kwa Waandishi hao  yaliyofanyika Kidongo Chekundu Zanzibar
Afisa Lishe Wilaya ya Kaskazini “A” Omar Saleh Machano akizungumza wakati  alipokua akiwasilisha mada ya changamoto za upungufu wa damu katika Wilaya wakati wa  mafunzo ya lishe kwa Waandishi wa Habari yaliyofanyika Kidongo Chekundu Zanzibar.
Daktari  bingwa wa magonjwa ya kina  mama Hospital ya Mnazimmoja Dkt. Zeana Abdul-aziz akichangia mada wakati wa mafunzo ya uhamasishaji lishe kwa Waandishi wa Habari yaliyofanyika Kidongo Chekundu Zanzibar.
 Daktari  bingwa wa magonjwa ya Wanawake Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja  Dkt.Sabra Salum   Machano  akichangia mada wakati wa mafunzo ya uhamasishaji lishe kwa Waandishi wa Habari yaliyofanyika Kidongo Chekundu Zanzibar.April 28,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Na Rahima Mohamed     Maelezo  28/04/2023

Jamii imetakiwa kuwapatia chakula bora mama wajamzito ili kuondokana na tatizo la upungufu wa damu mwilini wakati wa kujifungua.

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na wajawazito Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Zeyana Abdul-azizi wakati alipokuwa akitoa mafuzo kwa waandishi wa habari huko katika hospitali ya Kidongo chekundu.

Amesema tatizo la upungufu wa damu ni kubwa ambalo limekuwa likiwaathirika zaidi  wanawake hasa wajawazito  wakati wa kujifungua ndio wahitaji wa huduma ili kuokoa maisha ya mama na mtoto

Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi machi jumla ya kina mama 903 wamegundulika na matatizo ya upungufu wa damu kiwango ambacho kikubwa na kupelekea kuwapatia waginjwa kidogo kutokana na ufinyu wa huduma hiyo.

Amefahamisha kuwa kati ya wagonjwa hao waliolazimika kuongezewa huduma ya damu ni wagonjwa 75 ukilinganisha na ufinyu wa upatikanaji wa damu benki ya  damu.

Dr. Zeyana ameomba jamii  kujiandaa kabla na baada ya mama kupata ujazito kutumia vrutubisho vianavyoasaidia kujikinga na upungufu wa damu wakati wa kujifungua.

“Naiomba jamii ijiandae wakati mama anapotaka kubeba ujauzito tunashauri miezi 6 kabla mama watumie virutubishi ambavyo vitawasaidia kujikinga na tatizo la upungufu wa wakati wa kujifungua”, alieleza Dr. huyo.

Hata hivyo amewasisitiza kina mama na kina baba kuhudhuria kliniki kikamilifu kupata ushauri nasaha na kuanza tiba mapema ili kuepukana na tatizo la ukosefu wa  damu wakati wa kujifungua ili kunusuru maisha ya mama na mtoto.

Nae Afisa Lishe Wilaya ya Kaskazini A Omar Saleh Machano amesema upungufu wa damu ni tatizo la kiafya ambalo huathiri zaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa na wajawazito ambayo husababisha matokeo mabaya ikiwemo kujifungua kabla ya wakati, upungufu wa maadini  na kupelekea  vifo zaidi kwa kinamama.

Afisa huyo ameisisiza ulaji jamii  kuzingatia makundi sita ya vyakula ili kujenga afya bora pamoja na kuwaomba waandishi kuhamasisha jamii  kujenga mazingira wezeshi ya kuimarisha lishe na mtindo bora wa maisha pamoja na   ujio wa program ya utoaji dawa za kuongeza damu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.