Na.Rashid Omar OMKR.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanibar Mhe. Othman Masoud Othman,
amesema kwamba tatizo la uharibifu wa mazingira Zanzibar sio jambo lililoanza mara moja,
bali limetokea pole pole hadi kuweza kusababisha athari kubwa katika
maeneo mbali mbali ikiwemo uharibifu mkubwa
wa vyanzo vya maj nchini.
Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini
kwake Migombani mjini Zanzibar alipozungunza na Viongozi wa Taasisi za Dini na Jumuiya
zisizo za Serikali kuelezea mpango wa Serikali wa Kuirithisha Zanzibar kuwa ya
kijani ambapo mpango huo wa kitaifa unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Mhe. Makamu amesema kutokana na
hali hiyo hivi sasa uzalishaji wa maji
safi na salama umeshuka sana kutokana na vyanzo vingi vya maji kuharibika na
vyengine kukauka jamblo linalotaokana na
wananchi kuendelea kujenga taibia ya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa
miti ovyo.
Mhe. Makamu amefahamisha kwamba
kutokana na hali hiyo serikali imekuja na mpngo wenye mikakati shirikishi
itakayosaidia kubadili tabia za wananchi wa Zanzibar na kujajengea utamaduni mpya kwa watoto wote kupenda na kuheshimu miti sambamba
na kufahamu thamani ya kila miti nchini katika kuendeleza maisha bora ya wananchi.
Aidha emesema kwamba ukataji wa
miti na uharibifu wa maizingira pia hivi sasa umechangia kuwepo kasi kubwa ya maji ya bahari kuvamia
makaazi ya wananchi sambamba na kuwepo
mvua zisizotabirika huku hali ya joto ikongezeka na kuathiri maisha ya watu katika
maeneo mbali mbali.
Mhe. Othman amefahamisha mpango huo
wa serikali ambao tayari umepata Baraka katika ngazi zote za serikali
unakusudia kuwa jumuishi katika utekelezaji wake utakaowashirikisha wadau
mbali mbali wakiwemo watendaji wa taasisi za serikali, NGO’s pamoja na Taasisi
za dini wakiwemo wananchi wa kawaida.
Amefahamisha kwamba matumaini ya serikali
katika utekelezaji wa mpango huo kuwajengea utamaduni mpya wananchihasa vijana
kutambua thamani ya kuirithisha na kuiweka Zanzibar kuwa ya kijani ili
kuifanya nchi kutokuwa na athari kubwa inayotokana na uchafuzi wa manzingira kutokana na shughuli
za kibinaadamu.
Amesema kwamba kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2022
Zanzibar inaongezeko la watu takribani
laki sita, ikilinganishwa na sensa ya mwaka 2012, huku eneo lote la
ardhi ya Zanzibar likeendelea kuwa hekta
za mraba elfu mbili na mia
sita tu ambazo zinaendelea kupungua
kutokana na changamoto ya maji ya bahari kuvamia ardhi.
Mhe. Othman ameongeza kwamba Jumuiya
na taasiisi mbali ni vyema kushirikiana
na wananchi wote katika kuunga mkono
juhudi hizo malum kwa kushiriki katika
harakati mbali mbali ikwemo upandaji wa
miti katika maeneo tofauti
ikiwemo ya mikoko kuitunza na kudhibiti
ukataji ovyo wa miti ya aina zote nchini.
Mhe. Othman amesema pamoja na mambo
mengine katika utekelezaji wa mpango huo serikali kwa kushirikiana na wadau
mbali mbali itatoa elimu kwa wananchi sambamba na kushughulikia uzalishaji wa
miche ya miti mbali mbali pamoja na ushajiishaji wa wadau katika kuhamasisha
juu ya ushiriki wa kila mmoja katika kutekeleza mpango huo sambamba na kutoa
tunzo kwa kikundi , mtu ama taasisi zitakazofanya vyema zaidi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hya
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) ndugu Sheha Mjaja Juma amesema kwamba katika utekelezaji wa
mpango huo serikali inakusudia kupanda miti ya aina mbali mbali zaidi ya
milioni tatu kila mwaka.
Amfahamisha kwamba miti hiyo
itaoteshwa katika maeneo mbali mbali ya visiwa vya Unguja na Pemba kwa kupitia
ushiriki wa wadau mbali mbali wakiwemo wanafunzi, Jumiya za Kirai chini ya usimamizi wa Kamati maalum ya
serikali kuu ili kuhakikisha kwamba Zanzibar inarejeshewa hadhi ya uoto wa
asili ya kijani.
Mapema viongozi hao wa NGO na
taasisi za Dini walimueleza Mhe. Makamu kwamba taasisi zao zipo tayari
kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa mpango huo hasa katika suala la
kutafuta shughuli mbadala za kiuchumi kwa wananchi katika kuondokana na suala
la ukataji wa miti ovyo.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha habari leo tarehe 28.04.2023.
No comments:
Post a Comment