Habari za Punde

WCF YATWAA TUZO SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro leo Aprili 28, 2023.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya Mfuko Bora miongoni mwa Taasisi za Bima na Fidia wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako.

WCF imetwaa tuzo hiyo kwa kuwa  na Sera nzuri ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika Sekta ya Bima na Fidia kwa Wafanyakazi wakati wa Kilele cha Maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambapo kitaifa imefanyika mjini Morogoro.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako.

Akizungumza baada ya kutwaa tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Tuzo hiyo ni faraja kwa Wafanyakazi na Mfuko kwa ujumla imeonyesha jinsi mifumo ya kudhibiti ajali na magonjwa mahali pa kazi ni madhubuti.

“Hii inatupa matumaini na inatupa moyo zaidi kuendelea kuboresha maeneo ya kazi na kwakuwa WCF ni mdau mkubwa katika masuala haya hatuishii hapa tu kwa wafanyakazi wetu bali kwa wafanyakazi wengine ambao ni wadau wakubwa wa Mfuko.” Alifafanua.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,  Ajina na Wenye Ulemavu), Profesa Jamal Katundu (kushoto) akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro leo Aprili 28, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (Katikati), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya jamii, Mhe. Fastma Tawfiq (kulia kwa Profesa Ndalichako), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (mwenye koti jeusi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Jamal Katundu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF kwenye banda la Mfuko huo baada ya kutwaa tuzo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya kutwaa tuzo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kulia) na Meneja Tathmini na Usalama mahali pa Kazi WCF, Bi. Naanjela Msangi,


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.