Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mpango Akiwasili Bujubura Burundi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Bujumbura nchini Burundi na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Burundi Mheshimiwa Prosper Banzombaza leo tarehe 06 Mei 2023. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano kwaajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika Bujumbura nchini Burundi.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.