Wanachama wa Chamna cha ACT-Wazalendo wakifuatilia hutuba ya Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Taifa Mhe.Juma Duni haji huko katika viwanja vya alabama jimbo lakikwajuni mjini Unguja
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT –Wazalendo Zanzibar ambae ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka Wazanzibari wote kuendelea kuungana na kuwa wamoja katika kutetea haki sawa na kuendeleza kuijenga Zanzibar yenye umoja na maridhiano jambo litakaloleta Zanzibar mpya yenye neema na maendeleo kwa wote.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo Viwanja vya Alabama Jimbo la Kikwajuni wilaya ya mjini Unguja
katika mkutano wa tatu wa hadhara wa chama hicho Kwa upande wa Zanzibar.
Mkutano huo ni muendelezo wa
mikutano ya hadhara ya chama hicho tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuruhusu kuendelea kwa mikutano ya hadhara ya
vyama vya siasa nchini ambayo ilipigwa
marufuku kwa takribani kipindi cha miaka saba iliyopita.
Mhe. Othman amesema kwamba Maono ya
ACT ni kutetea na kujenga Zanzibar mpya yenye
neema na kujenga umoja bila kubaguana kwa kuzingatia kwamba
Zanzibar inaasili ya watu mchanganyiko
kutoka makabila na nchi tofauti
tokea kipindi cha kabla ya uhuru wa mwaka 1964.
Mhe, Makamu amefahamisha kwamba
katika kuthibitisha kuwepo hali hiyo ya
mchanganyiko mkubwa wa watu wa aina na makabila tofauti tokea asili, kesi ya mwanzo iliyofunguliwa
mahakamani katika kipindi cha kabla ya mwaka 1964 ni mama mmoja wa Zanzibar
kudai mahakamani haki za watoto wake aliozaa na mwanaume mwenye asili ya
kihidi.
Aidha amesema kwamba katika kipindi
cha kabla ya mwaka 1964 Zanzibar ilikuwa
na askari wapatao 707 ambao zaidi ya nusu walitoka katika makabila na nchi tofauti
ambao miongoni mwa hao ndio walioendelea kuishi Zanzibar hadi sasa na
kwamba hakuna sababu ya kubaguana.
Kwa upande mwengine Mhe. Othman
amesema kwamba chama hicho kitatimiza wajibu wake wa kuwasemea wananchi katika masuala mbali mbali yanayowahusu kupitia
mikutano ya hadhara bila kumuonea haya ama aibu mtu yoyote samabamba na kuwepo na
kutetea umoja na maridhiano ya kweli.
Kwa upande mwake Mwenyekiti wa
Chama hicho taifa Mhe. Juma Duni Haji (babu Juma), amewataka wazanzibar kuitumia
fursa ya kuundwa Kikosi kazi cha Kukusanya maoni ya Katiba mpya kwenda
kutoa maoni ya katiba inayohitajika itakayosaidia kuwepo pia muungano
wenye haki na maslahi sawa kwa pande
zote mbili.
Aidha Mwenyekiti huyo pia
alisisitiza haja ya wanzanibari kuitumia fursa hiyo katika kudai haki za
Zanzibar kwenye muungano kupitia katiba mpya ikatakayopendekezwa ili
kusaidia kufikia malengo ya chama hicho
kuleta umoja na maridhiano ya kweli miongoni mwa wazanzibari.
Amewakumbusha wazanzibari kukiunga
mkono chama hicho kwa vile chama chake kunaamini maridhiano ya
kweli na
kutetea umoja miongoni mwa wazanzibari jambo litakaloleta maslahi ya
kiuchumi na kuimarisha huduma biora za kijamii na kimaendeleo yakiwa ndio
malengo halisi ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Mapema Naibu Mkurugenzi wa Chama
hichi wa Haki za Binadamu na Makundi Maalum Pavu Abdalla Juma, amesema kwamba
Zanzibar imekabiliwa na changamoto kubwa ya kuwepo vitendo vya udhalilishaji
kwa wanawake na watoto jambo ambalo linaendelea kuleta athari kubwa kwa jamii
ya wazanzibar na kwamba kunahaja kubwa ya kuungana katika kupambania tatizo
hilo.
Mwisho
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Zanzibar kupitia Kitendo chake cha Habari leo tarehe 21.05.2023.
Kwa mawasiliano ya Haraka tafadhali
Piga simu.+255777424877 or
0774419740
No comments:
Post a Comment